Monday, June 25, 2012

MWENGE WA UHURU WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM, MIRADI YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 7 KUZINDULIWA.

 Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akiahidi mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadik kuupokea Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo miradi 11 itafunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es  Salam Saidi Meck Sadik (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Tatu Saidi Mussa leo jijini Dar es Salaam . Mwenge wa Uhuru umewasili  jijini  Dar es Salaam ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba.
 Wakimbiza Mwenge kitaifa wakiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Capt. Ernest Mwanossa (wa kwanza mbele)  wakianza safari kuelekea maeneo mbalimbali ya wilaya ya Temeke leo jijini Dar es Salaam.
 Askari kutoka jeshi la Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa sherehe za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam. 
 Vijana wa halaiki kutoka wilaya ya Temeke wakiimba wimbo maalum wa Mwenge wakati wa mapokezi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO


====  ============  =======



Mwenge wa Uhuru umewasili jijini DSM  leo na kupokewa na mamia ya wakazi wa Jiji. Mwenge huo uliwasili muda wa saa 4 asubuhi ukitokea kisiwani Pemba kusini, na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa D’salaam Mheshimiwa Mecky Sadick.


Akisoma risala ya Mkoa wa DSM Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alisema jumla ya miradi 27 itafunguliwa katika wilaya 3 za Mkoa wa huu. Alisema jumla ya miradi 11 itafunguliwa wilaya ya Temeke, Miradi 9 wilaya ya Ilala na miradi 7 wilaya ya Kinondoni.


Jumla ya thamani ya miradi yote itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru ni shilingi bilioni 7,911,501,171.


Ndugu Sadick alitoa mchanganuo wa gharama hizo kama ifuatavyo:-


Nguvu za wananchi ni shs: milioni 137, 859,100/-


Halmashauri shilingi bilioni 1, 389,296,587/-


Serikali Kuu shilingi milioni 69,872,500/-


Wahisani shilingi bilioni 6,314,472,984/-


Katika Risala ya utii kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Tanzania kila wilaya itatoa mchanganuo wa michango mbalimbali alisema Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa.Mwenge wa Uhuru leo [Jumanne] utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala na kesho utamaliza mbio zake wilaya ya Kinondoni, kabla ya kukabidhiwa kwa mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo.


Ujumbe wa mbio za Mwenge kwa mwaka huu ni, Sensa ya Watu na Makazi.

Mchakato wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na 

Mapambano dhidi ya dawa za kulevya na ukimwi.

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

Hiiii kina ras makunja wanaota moto?kweli baridi kali